RAIS ATAKIWA KUANGAZIA UTATA WA ARDHI ATAKAPOZURU TRANS NZOIA.


Serikali imetakiwa kuangazia kikamilifu swala la wakimbizi katika kaunti ya Trans nzoia.
Mbunge wa Kiminini Dkt Chris Wamalwa amesema kuwa swala la wakimbizi ni nyeti na iwapo litaangaziwa kwa wakati unaofaa basi maendeleo yataimarishwa hivyo kusukuma mbele uchumi wa kaunti hiyo.
Wamalwa amesema kuwa viongozi wa eneo hilo wataandaa kikao na rais Uhuru Kenyatta atakapozuru kaunti ya Trans nzoia ili kutafuta suluhu kwa tatizo hilo ambalo limekuwa kizungumkuti katika kaunti hiyo.
Wakati uo huo viongozi kutoka magharibi ya nchi wamehimiza kuwepo umoja miongoni mwa viongozi wakati rais Uhuru Kenyatta akitarajiwa kuzuru eneo hilo kuzindua miradi mbali mbali ya maendeleo.