RAIS ATAKIWA KUANGAZIA UPYA BEI YA ZAO LA MAHINDI.

Na Benson Aswani
Mbunge wa Endebess Dkt Robert Pukose amelalamikia bei duni ya zao la mahindi katika kanda ya Northrift akimtaka Rais Uhuru Kenyatta kungilia kati na kuhakikisha wakulima wanapoendelea na shuguli ya kuvuna mazao yao wanapata bei bora.
Akihutubu eneo la Chorlim eneo bunge la Endebes Kaunti ya Trans-Nzoia Dr Pukose amelalamikia kupanda maradufu kwa bei ya mbolea na gharama ya uzalishaji wa zao la mahindi akisema iwapo serikali haitaboresha bei ya zao hilo basi mkulima huenda akapata hasara na hata kukosa kuzalisha mahindi msimu ujao.
Wakati huo huo Dkt Pukose amemtaka mwenyekiti wa kamati ya Kilimo Katika bunge la Kitaifa Silas Tiren na mbunge wa Cherangani Joshua Kuttuny kuwatimizia wakulima ahadi ya bei ya shilingi 3,500 kwa kila gunia la kilo tisini la mahindi.