RAIS ATAKIWA KUANGAZIA SWALA LA UMILIKI WA ARDHI TRANS NZOIA.


Rais Uhuru Kenyatta ametakiwa kusuluhisha maswala ya dhuluma za kihistoria, umiliki wa ardhi na swala la maskwota katika kaunti ya Trans nzoia wakati atakapozuru kaunti hiyo katika ziara yake ya kaunti za eneo la magharibi ya nchi.
Kulingana na mwakilishi wadi ya Kinyoro Lawrence Mogosu, tume ya kutatua migogoro ya ardhi nchini haijatatua mizozo yoyote katika kaunti ya Trans nzoia tangu kubuniwa kwake hivyo kuwaacha wenyeji wengi bila makao na kuendelea kusakamwa na umasikini
Aidha mogosu amemtaka rais Kenyatta kuzindua ujenzi wa barabara ya lami katika eneo bunge la saboti akisema kuwa tangu taifa kujinyakulia uhuru eneo bunge hilo halijawahi kupata lami huku maeneo mengine nchini yakipata zaidi ya kilomita 30 ya lami.