RAIS ATAKIWA KUANGAZIA HALI TETE YA USALAMA ENEO LA KERIO VALLEY.


Baadhi ya viongozi kwenye kaunti ya elgeyo marakwet wamemshutumu rais uhuru kenyatta kwa kusalia kimya kuhusu swala la utovu wa usalama kwenye eneo la bonde la kerio ambalo limechangiwa na wizi wa mifugo.
Akiongea na wanahabari mbunge wa keiyo kusini daniel rono amemtaka rais kenyatta kujitiokeza wazi na kuzungumzia hali tata ya usalama katika bonde hilo na hata kufanya ziara ili kuwahakikishia wakazi usalama wao.
Rono amesema kuwa uvamizi wa mara kwa mara eneo hilo umepelekea maafa ya watu wengi wasio na hatia huku wengine wakizama kwenye lindi la umaskini baada ya wavamizi kuiba mifugo wao wote.
Rono aidha amesema kuwa kama viongozi wataandaa maandamano hadi kwenye afisi ya rais jijini nairobi ili kuishinikiza serikali kushughulikia tatizo la ukosefu wa usalama kwenye bonde la kerio.