‘RAILA HATAMBI POKOT MAGHARIBI’, WASEMA WANDANI WA RUTO.

Na Benson Aswani
Wandani wa naibu rais William Ruto katika kaunti hii ya Pokot magharibi wamepuuzilia mbali miito ya baadhi ya viongozi kaunti hii kwa wakazi kumuunga mkono kinara wa chama cha ODM Raila Odinga katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Wakiongozwa na mbunge wa Sigor Peter Lochakapong, viongozi hao wamesema kuwa itakuwa vigumu kwa Raila kuungwa mkono katika kaunti hii ikizingatiwa rekodi yake ya kutembelea kaunti hii ikilinganishwa na naibu rais William Ruto.
Lochakapong ametoa wito kwa wakazi kuwa makini wakati huu wa kampeni za kisiasa na kutokubali kuhadaiwa na viongozi wanaolenga kuwashawishi kuwaunga mkono na badala yake kufanya uamuzi wa busara kwa kuegemea viongozi ambao uongozi wao utakuwa na manufaa kwa kaunti hii.