RAILA ATUA POKOT MAGHARIBI KATIKA KAMPENI YA AZIMIO LA UMOJA.

Na Benson Aswani
Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga yuko katika kaunti hii ya Pokot magharibi katika misururu ya kampeni yake ya azimio la umoja.
Raila ameanza ziara yake kwa kukutana na wajumbe wa chama cha ODM katika uwanja wa kishaunet kabla ya kuhutubia umma katika bustani ya Chelang’a mjini Makutano.
Raila yuko katika ziara ya siku tatu eneo la magharibi ya nchi na kaskazini mwa bonde la ufa kuhimiza umoja miongoni mwa wakenya huku pia akitumia fursa hiyo kujipigia debe katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Ziara yake ilianzia katika kaunti ya Trans nzoia na kisha eneo la Butere kaunti ya Kakamega ambako amesisitiza sera yake ya kutoa shilingi alfu sita kwa wakenya kutoka jamii masikini huku akiwapuuzilia mbali wanaokosoa sera hiyo.