RAILA ASUTWA VIKALI KWA KUWA ‘KISIRANI’ KWA SERIKALI ZA HAPA NCHINI.

Viongozi wanaoegemea mrengo wa Kenya kwanza wameendelea kumsuta kinara wa chama cha muungano wa azimio la umoja one Kenya Raila Odinga kwa kuendeleza maandamano dhidi ya serikali ya rais William Ruto.

Mbunge wa Sigor katika kaunti ya Pokot magharibi Peter Lochakapong alisema kwamba Raila amekuwa tatizo kwa serikali za hapa nchini kwa muda sasa kwa kuandaa maandamano ya kila mara na kuhujumu shughuli mbali mbali za wakenya akimtaka kutumia mbinu mbadala za kikatiba kuendeleza harakati zake.

“Kwa hii miaka yote tumekuwa tukisikia tu Raila ndiye anasumbua watu, anaitisha maandamano na kutatiza shughuli za wananchi wa kawaida. Raila anapasa kufahamu kwamba Kenya ina katiba na anafaa kuheshimu katiba na kufuata taratibu zinazostahili kwa kuchukua hatua yoyote.” Alisema Lochakapong.

Lochakapong alimtaka rais William Ruto pamoja na taasisi mbali mbali za kikatiba kuchukua hatua dhidi ya viongozi wote wa upinzani ambao wanakwenda kinyume cha sheria kupitia mandamano hayo wakiongozwa na kinara wao Raila Odinga.

“Kwa hivyo nasema kwamba kazi sasa ni kwa rais William Ruto na wote ambao tumewapa nafasi na nyadhifa mbali mbali za kuona kwamba katiba na sheria zinazingatiwa hapa nchini, kuhakikisha kwamba hatua inachukuliwa kwa mtu yeyote ambaye atavunja sheria akiwemo Raila Odinga.” Alisema.

[wp_radio_player]