PUKOSE ASHUTUMIWA KWA KUDHALILISHA BARAZA LA WAZEE.
Mbunge wa Endebes kaunti ya Trans nzoia Robert Pukose ametakiwa kuomba msamaha kufuatia madai ya kulidhalilisha baraza la wazee wa jamii la sabaot katika kaunti hiyo wakati wa mkutano na mshirikishi wa utawala wa bonde la ufa George Natembeya juma lililopita.
Wakiongozwa na aliyekuwa naibu wa meya wa mji wa Kitale Pius Arap Kauka, wazee hao wamesema mkutano baina yao na Natembeya eneo la soi kwenye kaunti ya Uasin Gishu ulikuwa wa kujadili swala la kudumisha amani pamoja na siasa za mwaka ujao.
Wakati uo huo Arap kauka ameutaja mkataba wa maelewano wa amani maarufu Mabanga peace accord wa mwaka 2011 uliotiwa saini na jamii tatu mbele ya aliyekuwa makamo wa rais Kalonzo musyoka kuwa nguzo muhimu ambao unafaa kudumishwa wakati wa uchaguzi mkuu ujao.