POLISI WAMEOKOA MSHUKIWA WA WIZI KAUNTI YA TRANSNZOIA

Maafisa wa Polisi mjini kitale wamelazimika kutumia Vitoza machozi kuwatawanya Wahudumu wa Bodaboda waliojawa Gadhabu ambao wamekuwa wakimpiga mshukiwa wa wizi wa pikipiki kwa mawe na vifaa Butu.

Mmoja wa walioshuhudia kisa hicho Simon Mainge amesema visa vya Wizi wa Pikipiki vimekithiri huku waliochukua Mikopo kununua Pkipiki wakikadiria hasara ya mali yao kunadiwa

Mainge amesema kwamba katika visa hivyo waendeshaji Pikipiki hujeruhiwa na hata wakati mwingine huuliwa na wezi hao wakimabavu waliojihami kwa Panga Nyundo na vifaa vingine hatari

Ikumbukwe majuma mawili yaliyopita maafisa wa Polisi wa kituo cha endebes walifanikiwa kumtia nguvuni mshukiwa mkuu mwanammke kwa kupatikana na pikpiki na nambari za usajili arobaini

[wp_radio_player]