POLISI WALAUMIWA KWA KUWAKAMATA KIHOLELA WAKAZI MAKUTANO.polisi
Wakazi mjini makutano kaunti hii ya Pokot magharibi wameendelea kulalamikia kile wamedai kukamatwa kiholela na maafisa wa polisi kwa madai ya kutekeleza kanuni za kukabili msambao wa virusi vya corona.
Wakizungumza baada ya maafisa wa polisi kuwakamata watu kadhaa kwa kutovalia maski, wakazi hao wakiongozwa na Dennis Kapchok wamedai kuwa polisi wanatumia fursa hiyo kutafuta fedha kutoka kwa wakazi kwa kisingizio cha kutekeleza kanuni hizo.
Wakazi hao sasa wanawataka polisi kuwahamasisha wakazi kuhusu umuhimu wa kuzingatia kanuni za kukabili msambao wa virusi vya corona iwapo wanataka kuzingatiwa kanuni hizo badala ya kuwakamata kiholela kwa lengo la kutoa fedha kwao.