POLISI KANYARKWAT POKOT MAGHARIBI WALAUMIWA KWA KUWAHANGAISHA WENYEJI.

Na Benson Aswani
Polisi eneo la Kanyarkwat katika kaunti hii ya Pokot magharibi wamelaumiwa pakubwa kwa kuwahangaisha wakazi wa maeneo hayo hasa nyakati za usiku.
Mbunge wa Kapenguria Samwel Moroto amesema kuwa licha ya kuondolewa amri ya kutokuwa nje nyakati za uskiu baada ya kupungua maambukizi ya virusi vya corona, maafisa wa polisi wameendelea kuwahangaisha wakazi eneo hilo ambao wanatekeleza shughuli zao nyakati za usiku.
Moroto anadai kuwa wakazi wa eneo hilo wamekuwa wakiishi kwa amani baada ya kusuluhisha mizozo ambayo ilishuhjudiwa awali hasa na wenzao kutoka kaunti jirani ya Trans nzoia ila sasa maafisa wa polisi wamekuwa tatizo kwao akiwataka wakuu wa usalama eneo hilo kuhakikisha wanadfhibiti maafisa wao.