POKOT MAGHARIBI YASAJILI ASILIMI 33 YA WAPIGA KURA WAPYA.

Na Benson Aswani
Zoezi la usajili wa wapiga kura likiwa limekamilika kulingana na mipangilio ya tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kaunti hii ya Pokot magharibi ilikuwa imewasajili jumla ya wapiga kura alfu 19,400 kufikia tarehe 31 mwezi octoba.
Haya ni kwa mujibu wa takwimu kutoka tume ya IEBC kaunti hii ya Pokot magharibi ambapo kulingana na meneja wa tume hiyo John Mwangi idadi hiyo ni asilimia 33 pekee ya jumla ya wapiga kura wapya alfu 58 ambao walikuwa wamelengwa kusajiliwa kufikia mwisho wa zoezi hilo.
Eneo bunge la Kapenguria linaongoza kwa kusajili wapiga kura wapya alfu 5,459 likifuatiwa na eneo bunge la pokot kusini kwa wapiga kura alfu 5,185, sigor alfu 4,963 huku kacheliba ikisajili wapiga kura alfu 3,793 kufikia tarehe 31 mwezi octoba.
Mwangi amewataka wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi kuchukulia kwa uzito zoezi la usajili wa wapiga kura linapotangazwa akisema kuwa ni muhimu katika kubaini mustakabali wa taifa kwani ni kupitia niia hiyo tu ndipo wataweza kuchagua uongozi wanaotaka