POKOT MAGHARIBI YAKABILIWA NA HATARI YA BAA LA NJAA.


Huenda visa vya utapiamlo vikaongezeka hata zaidi katika kaunti hii ya pokot magharibi kutokana na uhaba wa chakula ambao huenda ukashuhudiwa hivi karibuni.
Haya ni kulingana na afisa katika shirika la Action against hunger Salome Tsindori ambaye amesema kuwa licha ya kuwa kaunti hii haikuorodheshwa miongoni mwa kaunti ambako kulitangazwa njaa kuwa janga, pokot magharibi inakabiliwa na hatari ya kukumbwa na njaa kutokana na hali kuwa mimea ya wakulima wengi iliathirika kutokana na ukame ulioshuhudiwa mapema mwaka huu.
Amesema kutokana na hali hii familia nyingi hazitakuwa na mavubo ya kutosha na huenda zikakumbwa na ukosefu wa chakula karibuni hali ambayo ityapelekea visa vingi vya utapiamlo miongoni mwa watoto.
Tsindori amesema kuwa shirika hilo limeanzisha miradi mbali mbali ya kilimo hasa kwa akina mama maeneo ya vijijini ambayo itasaidia kuhakikisha hawakabiliwi na makali ya njaa katika juhudi za kuepuka kukithiri visa vya utapiamlo kutokana na uhaba wa chakula.