POGHISIO ATOA WITO WA KUZIDISHWA JUHUDI ZA KUTWAA SILAHA HARAMU MAENEO KAME.


Seneta wa kaunti hii ya Pokot magharibi Samwel Poghisio ameelezea kusikitishwa na umiliki wa hali ya juu wa bunduki miongoni mwa raia nchini hasa maeneo kame.
Akirejelea kisa cha kujipiga risasi na kuaga dunia mwanawe mbunge maalum David Ole Sankok, Poghisio amesema kuwa licha ya juhudi za serikali kuhakikisha kuwa bunduki zinazomilikiwa kinyume cha sheria zinaondolewa miongoni mwa wananchi, visa vya wananchi kumiliki bunduki vimekithiri nchini.
Hata hivyo Poghisio ametumia fursa hiyo kutuma risala za rambi rambi kwa familia ya mbunge huyo kwa kumpoteza mpendwa wao.
Poghisio ametoa wito wa ushirikiano baina ya wadau mbali mbali ili kuhakikisha kuwa juhudi za kutwaa silaha zinazomilikiwa kinyume cha sheria zinafanikishwa na kuwahakikishia usalama wakazi wa maeneo haya ambayo yameshuhudiwa utovu wa usalama kwa muda sasa.