POGHISIO APUUZILIA MBALI HATUA YA KUP KUJIUNGA NA ODM.

Na Benson Aswani
Seneta wa kaunti hii ya Pokot magharibi Samwel Poghisio amepuuzilia mbali hatua ya chama cha KUP kutangaza kujiunga na chama cha ODM wakati wa ziara ya azimio la umoja ya kinara wa ODM Raila Odinga hiyo jana katika kaunti hii.
Akizungumza na kituo hiki Poghisio ambaye pia ni kiongozi wa wengi katika bunge la seneti amesema kuwa hatua hiyo ilikuwa tu ni mbinu ya viongozi wa chama hicho kuonyesha kuwa chama hicho kina umaarufu katika kaunti hii swala analosema lilifeli kuafikia malengo yao.
Wakati uo huo Poghisio amejitenga na madai kuwa anapanga kujiunga na chama hicho akishikilia kuwa yeye nia mwanachama wa KANU na uwepo wake katika hafla hiyo ilikuwa tu kumpokea Raila kutokana na heshima yake kwake, huku akisisitiza kuwa hatajiunga na kile ametaja kuwa vyama visivyo na sura ya kitaifa.