POGHISIO APUUZA MADAI YA KUWEPO MPANGO WA KUMUUNGA MGOMBA MMOJA WA UGAVANA POKOT MAGHARIBI CHINI YA AZIMIO.


Seneta wa kaunti hii ya Pokot magharibi Samwel Poghisio amepuuzilia mbali madai kuwa kaunti hii imetengewa mgombea mmoja chini ya muungano wa azimio la umoja one Kenya kwa wadhifa wa ugavana.
Poghisio amesema kuwa kila chama kilicho chini ya muungano huo kaunti hii kitaunga mkono mgombea wake wa ugavana na kukutanishwa na mgombea urais ambaye vyama vyote chini ya muungano huo vitamuunga mkono Raila Odinga.
Poghisio amesema tayari mgombea ugavana kupitia chama cha KANU Nicholas Atudonyang tayari amepewa tiketi ya kuwania wadhifa huo.
Ametaja madai hayo kuwa propaganda ambazo zinaenezwa na chama cha KUP kwa nia ya kumpigia debe gavana wa sasa John Lonyangapuo machoni pa wakazi akisema kamwe hawatamuunga gavana lonyangapuo kuwania awamu ya pili ya ugavana kaunti hii.