POGHISIO AMTAKA RAIS KUZURU POKOT MAGHARIBI KATIKA ZIARA YAKE YA BONDE LA UFA.


Seneta wa kaunti hii ya Pokot magharibi Samwel Poghisio amesema kuwa mazungumzo yanaendelea kuhakikisha kuwa rais uhuru kenyatta anafika kaunti hii ya Pokot magharibi atakapozuru eneo la kaskazini mwa bonde la ufa.
Poghisio amesema kuwa japo kaunti hii haiko kwenye orodha ya kaunti ambazo rais Kenyatta anatarajiwa kuzuru, wanaweka mikakati ya kuhakikisha anakutana na wakazi wa kaunti hii, na iwapo hilo halitowezekana basi wapange ziara rasmi ya rais kukagua miradi ambaye imetekelezwa kaunti hii.
Wakati uo huo Poghisio ametetea mipango ya kubuniwa muungano baina ya chama cha Jubilee na ODM na kudokeza uwezekano wa muungano huo kufanya kazi na ule wa one kenya alliance katika kuhakikisha chama cha uda kinanyimwa fursa ya kupata uongozi wa taifa.