POGHISIO AKOSOA WAPINZANI WAKE WANAOGOMBEA USENETA POKOT MAGHARIBI

Seneta wa kaunti hii ya Pokot magharibi Samwel Poghisio amepuuzilia mbali wapinzani wake ambao wametangaza kuwania kiti hicho katika uchaguzi mkuu wa mwezi agosti mwaka huu.
Akizungumza katika mahojiano ya kipekee na kituo hiki Poghisio amedai kuwa baadhi ya wagombea ambao wanamezea mate kiti hicho wanafanya hivyo kutokana na misukumo ya kisiasa kwa nia ya kumpinga wala si kuwahudumia wananchi.
Poghisio amesema kuwa ametekeleza mengi katika kuhakikisha kuwa kaunti hii inatengewa mgao zaidi, akielezea kushangazwa na watakachotekeleza waliotangaza nia ya kugombea kiti hicho.
Wakati uo huo Poghisio ameendelea kukosoa uongozi wa gavana Joh Lonyangapuo kwa kile amedai licha ya juhudi zake kuhakikisha kwamba kaunti hii inatengewa mgao zaidi serikali gavana Lonyangapuo imefuja fedha hizo kupitia uporaji.