POGHISIO AKOSOA MPANGO WA KUWAHAMISHA WALIMU WAKUU.


Seneta wa kaunti hii ya Pokot magharibi Samwel Poghisio amelalamikia kudorora viwango vya elimu kutokana na kile amedai kutolewa walimu wa kaunti hii katika mpango wa kuwahamisha walimu kufunza katika kaunti zingine.
Haya ni kwa kujibu wa seneta wa kaunti hii Samwel Poghisio ambaye amesema kuwa tayari kaunti hii ilisalia nyuma kwa maswala ya maendeleo ikilinganishwa na kaunti zingine na hatua ya kuwahamisha walimu ambao wangeiwezesha kufikia viwango vya kaunti zingine kielimu ni kuhujumu pakubwa juhudi hizo.
Poghisio ameitaka idara ya elimu kuangazia swala hilo akisema kuwa kaunti hii haikuwa tayari kwa mpango wa kupewa walimu uhamisho yani delocalisation kwani walimu wanaotumwa kaunti hii kutoka nje huchukua muda mchache sana shuleni hali ambayo imeathiri viwango vya elimu.
Wakati uo huo Poghisio amekosoa mtaala wa umilisi CBC akisema ni ghali mno kwa wazazi wenye mapato ya chini akitaja pia swala la miundo msingi kuwa kikwazo kwa utekelezwaji wake huku akitaka idara ya elimu kuuangazia upya.