POGHISIO AKASHIFU UVAMIZI UNAOSHUHUDIWA MIPAKANI PA POKOT MAGHARIBI NA TURKANA.


Seneta wa Kaunti ya Pokot Magharibi Samuel Poghisio ameukashifu visa vya uvamizi ambavyo vimeendelea kushuhudiwa katika Eneo la Kainuk mipakani pa Kaunti hii ya Pokot Magharibi na Turkana, akisema kwamba inashangaza kushuhudiwa kwa uvamizi huo baada ya miaka kadhaa ya amani.
Poghisio ametoa wito kwa Idara ya Usalama wa ndani kuchukua hatua ya kuzipa ulinzi shule kadhaa katika maeneo hayo ili kuwapa wanafunzi fursa ya kujitayarisha kikamilifu katika mitihani ya KCSE na KCPE.
Ametumia fursa hiyo kuwashauri wakazi wa maeneo hayo kujihusisha na kilimo biashara badala ya kufikiria kuhusu ufugaji pekee.