POGHISIO AKASHIFU MPANGO WA KUMBADUA AFISINI SPIKA MKENYANG.


Seneta wa kaunti hii ya pokot magharibi samwel poghisio ameshutumu juhudi ambazo zinaendelezwa na wabunge wa bunge la kaunti hii ya pokot magharibi kumwondoa mamlakani spika Catherine Mukenyang.
Akizungumza na kituo hiki Poghisio amewasuta baadhi ya viongozi wa kisiasa katika kaunti hii kwa kile amedai kuwa wamehonga baadhi ya waakilishi wadi katika juhudi za kuhakikisha Mukenyang anaondolewa afisini.
Wakati uo huo Poghisio amesuta uongozi wa kaunti hii kwa kile amedai unatumia fedha ambazo zilistahili kutumika kuongeza dawa katika vituo vya afya na kufadhili elimu kupitia fedha za basari kufadhili juhudi za kumbadua afisini spika Mukenyang.