POGHISIO AHIMIZA KUZINGATIWA TAMADUNI ZA JAMII YA POKOT.


Ipo haja kwa viongozi mbali mbali ambao wanachaguliwa kuongoza kaunti hii ya Pokot magharibi kuzingatia pakubwa swala la tamaduni za jamii ya kaunti hii.
Akizungumza baada ya kuhudhuria sherehe ya kitamaduni ya Sentaa eneo la muino katika kaunti hii ya Pokot magharibi, seneta Samwel Poghisio amesema kuwa tamaduni hizo zina umuhimu mkubwa kwa wakazi iwapo zitazingatiwa kikamilifu.
Poghisio amedai kuwa huenda majanga ambayo yamekumba kaunti hii katika kipindi cha uongozi wa gavana John Lonyangapuo yametokana na kutozingatia kwake umuhimu wa tamaduni za jamii jinsi alivyofanya mtangulizi wake.
Poghisio amesema kuwa sherehe hiyo ina umuhimu mkubwa zaidi kwa wakazi wa kaunti hii ikiwemo kuhakikisha umoja, akielezea haja ya kuwekwa mikakati ya kuhakikisha kuwa wakazi wengi hata kutoka kaunti jirani wanahudhuria.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na mwaniaji kiti cha mwakilishi wadi ya Weiwei David Moiben ambaye aidha amesisitiza haja ya kuzingatiwa kikamilifu kama ishara ya umoja wa wakazi wa kaunti hii na majirani zake.

[wp_radio_player]