PENDEKEZO LA KUFANYIA WANAFUNZI VIPIMO SHULENI LAENDELEA KUIBUA HISIA.

NA BENSON ASWANI
Hisia mseto zimeendelea kuibuliwa miongoni mwa wadau katika sekta ya elimu kuhusu pendekezo la kufanyia vipimo wanafunzi kutoka shule ambazo ziliripoti kuteketezwa majengo ya shule ili kubaini iwapo baadhi yao wanatumia pombe na dawa za kulevya.
Wa hivi punde kutolea hisia agizo hilo la waziri wa elimu Prof George Magoha ni mwalimu mkuu wa shule ya upili ya LCK Chepareria katika kaunti hii ya Pokot magharibi John Kapoyong ambaye ameelezea kuunga mkono agizo hilo akisema kuwa hatua hiyo itasaidia kukabili utovu wa nidhamu miongoni mwa wanafunzi.
Kuhusu mitihani ya kitaifa inayotarajiwa kuanza mwezi machi mwaka huu, Kapoyong amewahakikishia wazazi wa shule hiyo kuwa mikakati ya kutosha imewekwa kuhakikisha kuwa shule hiyo inafanya vyema katika mtihani wa kitaifa kwa kidato cha nne KCSE.