OPARESHENI YAENDELEA KUTEKELEZWA KAPEDO HUKU WATU SABA WAKIKAMATWA NA SILAHA HARAMU KUTWALIWA


Mshirikishi wa serikali eneo la Bonde la Ufa George Natembeya amesema kuwa kufiki sasa watu 7 wametiwa mbaroni na maafisa wa polisi katika oparesheni inayoendelezwa eneo la Kapedo mpakani pa kaunti za Baringo na Turkana.
Akizungumza na wanahabari katika kaunti ya Nakuru, Natembeya amesema kuwa kuna idadi ambayo hakutaja ya bunduki ambayo tayari zimetwaliwa kutoka mikoni mwa wahalifu kufikia sasa.
Natembeya aidha amesema kuwa shule za msingi na hata za upili zitafunguliwa wiki ijayo kule kapedo ili wanafunzi waweze kujiandaa kwa mitihani ya kitaifa.