OPARESHENI KALI YAANZISHWA YA KUHAKIKISHA WANAFUNZI WOTE WANAPELEKWA SHULENI KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI
Zaidi ya wanafunzi alfu 4 hawajaripoti shuleni tangu kuanza zoezi la kuwasajili wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza katika kaunti hii ya Pokot magharibi.
Haya ni kwa mujibu wa kamishina wa kaunti hii Apolo Okelo ambaye amesema kuwa licha ya agizo la serikali kuhakikisha asilimia 100 ya wanafunzi hao wanajiunga na kidato cha kwanza, kaunti hii haijaafikia hilo.
Apolo amesema kuwa wameanzisha oparesheni ya wiki mbili ya kuhakikisha kuwa wanafunzi hao wanapatikana na kupelekwa shuleni.
Aidha Apolo ametoa wito kwa wadau ikiwemo wazazi na walimu kushirikiana na maafisa wanaoendeleza shughuli hiyo ili kuhakikisha wanafunzi hao wanapatikana na kuwasilishwa shuleni.