OPARANYA ATAKIWA KUIMARISHA HALI YA HOSPITALI YA WILAYA YA MATUNGU

Mbunge wa Matungu kaunti ya Kakamega Oscar Nabulindo amelalamikia huduma duni zinazotolewa katika hospitali ya wilaya ya Matungu akiilaumu serikali ya kaunti ya Kakamega kwa kuitelekeza hospitali hiyo.

Nabulindo amesema kuwa hospitali hiyo haina dawa za kutosha, vifaa vya kutosha kwa wahudumu wa afya kutoa huduma zinazostahili, mbali na kutokuwa na mtaalam wa matibabu hata mmoja.

Ametoa wito kwa serikali ya kaunti hiyo chini ya gavana Wyclife Oparanya kuhakikisha hospitali hiyo inashughulikiwa ikizingatiwa idadi kubwa ya wagonjwa wanaofika kutafuta huduma za matibabu.

[wp_radio_player]