ONYO YATOLEWA KWA WANAOVURUGA MIKUTANO YA KISIASA TRANS NZOIA.

Na Benson Aswani
Mshirikishi wa serikali eneo la bonde la ufa George Natembeya ameonya vikali dhidi ya vijana kutumika kuvuruga mikutano inayoandaliwa na wagombea nyadhifa mbali mbali katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Akizungumza katika hafla moja ya mchango eneo la Babton kaunti ya Trans nzoia, Natembeya ambaye pia ametanga nia ya kugombea ugavana katika kaunti hiyo amesema kuwa hulka hiyo ya kuwakosea heshima viongozi wengine haitakubalika.
Natembeya ametumia fursa hiyo kutoa mwito kwa wakazi wa kaunti ya Trans nzoia kudumisha amani na umoja wakati taifa linapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.