ONYO YATOLEWA KWA WABAKAJI BUKWO.


Visa vya mimba za mapema, ndoa za mapema pamoja na ubakaji miongoni mwa watoto wa kike vimeripotiwa kukithiri mipakani pa kaunti hii ya Pokot magharibi na taifa jirani la Uganda.
Akizungumza katika mahojiano na kituo hiki kamishina wa wilaya ya Bukwo Samwel Kiprop alisema kwamba hatima ya mtoto wa kike maeneo hayo imo hatarini iwapo hatua mwafaka hazitachukuliwa dhidi ya uovu huo.
Ni kutokana na hali hii ambapo kamishina huyo alitoa onyo kali kwa wanaohusika uovu huo akisema kuwa atakayepatikana atakabiliwa vikali kulingana na sheria za taifa hilo.
Wakati uo huo Kiprop aliwataka wazazi maeneo hayo kutowaweka wanao katika hatari ya kukumbwa na hali hiyo ikiwemo kuwatuma nje nyakati za usiku mbali na kuhakikisha kwamba wanao wanahudhuria masomo.
Aidha alidokeza mipango ya kuanzishwa oparesheni ya kuwasaka watoto ambao hawahudhurii masomo shuleni akionya kuchukuliwa hatua wazazi ambao watapatikana na wanao nyumbani.