ONYO KALI YATOLEWA DHIDI YA UKEKETAJI KACHELIBA

Naibu kamishana wa eneo la Kacheliba kaunti ya Pokot Magharibi David Mugutsu amewaonya vikali watu walio na nia ya kuwakeketa na kuwaoza wasichana mapema hasa wanafunzi wakati huu wa likizo.

Mugutsu amewataka wazazi kuwatunza vyema wanao ili kuhakikisha kuwa wanarejea shuleni wakiwa katika hali nzuri akisisitiza kuwa watahakikisha hakuna kisa chochote cha kukeketwa au kuozwa mapema watoto wa kike eneo hilo.

Ikumbukwe wiki iliyopita wanaume wawili walikamatwa na maafisa wa polisi katika eneo bunge la Kacheliba baada ya kuwaruhusu wake zao kukeketwa kisiri, baadaye wakapatikana wakiwa hali mahututi baada ya kuvuja damu nyingi.