ONGEZEKO LA PEMBEJEO ZA KILIMO NA BEI YA MAFUTA LAZUA HOFU MIONGONI MWA WAKULIMA TRANS NZOIA

Kuendelea kupanda kwa bei ya pembejeo na kuongezwa kwa bei ya mafuta msimu huu wa upanzi huenda kukapelekea wakulima wengi kushindwa kumudu gharama ya kilimo, hivyo kuathiri pakubwa uzalishaji wa chakula nchini mwaka huu.

Akihutubu baada ya kutoa msaada wa magunia 600 ya mbolea kwa wakulima, mwakilishi wadi ya bidii kaunti ya Trans-Nzoia Peter Waswa amesema hatua hiyo itapelekea wakulima wengi kupanda mimea bila mbolea hivyo kuathiri viwango vya mazao.

Aidha Waswa ametoa wito kwa serikali kuu na zile za kaunti kungilia kati na kuwanusuru wakulima kwa kutenga fedha za kutosha ili kufadhili shughuli za kilimo nchini kama njia moja ya kukabili ongezekoa la bei ya chakula kwa wananchi mbali na uagizaji wa chakula kutoka mataifa ya kigeni.