OKA YATARAJIWA KUZURU KAUNTI YA TRANS NZOIA WIKENDI HII.

Vinara wa one Kenya alliance OKA wanatarajiwa kuizuru kaunti ya Trans nzoia hapo kesho kufanya misururu ya mikutano kwa lengo la kuwashawishi wakazi wa kaunti hiyo kumpigia kura mmoja wao watakapoafikiana kupeperusha bendera ya urais mwaka ujao.
Katibu mkuu wa chama cha Ford Kenya katika kaunti ya Trans nzoia Joseph Pepela amesema vinara wa OKA watatumia fursa hiyo kuangazia changamoto zinazomkumba mkenya wa kawaida.
Mmoja wa viongozi wa chama hicho susan nakhumicha na mwakilishi wa wadi ya sitatunga Daniel kaburu wamesema mkutano mkuu utafanyika mjini kitale.
Eneo hilo la transnzoia linawapiga kura takriban alfu miatatu sabini na mbili miasita hamsini na sita.