OKA YATAKIWA KUTENGENEZA MUUNGANO NA RAILA ODINGA.

Na Benson Aswani
Seneta wa kaunti hii ya Pokot magharibi Samwel Poghisio ametoa wito kwa viongozi wa muungano wa one Kenya alliance OKA kusalia pamoja uchaguzi mkuu wa mwaka ujao ukiendelea kukaribia.
Akizungumzia minong’ono kuhusu uwepo wa migawanyiko miongoni mwa viongozi wa muungano huo, Poghisio amesema kuwa itakuwa vigumu kwa kinara yeyote kutoka muungano huo kushinda katika uchaguzi mkuu ujao iwapo ataamua kwenda peke yake.
Hata hivyo poghisio amesema kuwa itakuwa bora zaidi iwapo muungano huo utaungana na kinara wa ODM Raila Odinga kuelekea uchaguzi ili kubuni muungano wa kisiasa wenye nguvu zaidi na kuwa na hakikisho la kutwaa uongozi wa taifa.
Poghisio amesema vinara wa muungano huo hawajaafikiana kuhusu ni nani atakaye peperusha bendera ya muungano huo katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao kutokana na misimamo mikali kutoka pande zote husika.