OKA YAJITETEA KUHUSIANA NA MADAI KUWA NI MUUNGANO WA KIKABILA.


Mshirikishi wa kitaifa wa muungano wa One Kenya Alliance Ferdinand Wanyonyi amekosoa vikali matamshi yaliyotolewa na naibu rais William Ruto kuwa muungano huo ni wa kikabila.
Wanyonyi amesema kuwa malengo ya OKA ni kujenga umoja kupitia uongozi wenye sura ya kitaifa, kuimarisha uchumi, kuhakikisha asilimia isiyopungua 35 ya raslimali za kitaifa inagawanywa kwa usawa na kupiga vita ufisadi wala si kupigia debe ukabila.
Wakati uo huo wanyonyi ambaye pia ni mbunge wa Kwanza katika kaunti ya Trans nzoia amemrai rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto kusuluhisha tofauti zao za kisiasa.