ODM YAPANGA MIKAKATI YA KUIMARISHA UMAARUFU WAKE


Chama cha ODM kinatarajiwa kurejelea misururu ya mikutano yake nchini ili kukabili uwezekano wa kuimarika kwa ushawishi wa kisiasa wa naibu wa rais daktari William Ruto katika maeneo mbali mbali ya nchi.
Junet Muhamed ambaye ni mbunge wa Suna Mashariki na mkurugenzi wa uchaguzi katika chama hicho cha ODM amesema kuwa wataandaa ziara nchini kote huku wakizingatia kanuni za wizara ya afya katika kukabili maambukizi ya covid-19.
Aidha Junet ameongeza kuwa chama cha ODM kinatarajia kuandaa makongamano nane ya wajumbe wa chama hicho katika kaunti mbalimbali kuanzia mwezi Machi huku kongamano la kitaifa likiandaliwa mwezi juni mwaka huu wa 2021.
Kwa mujibu wa Junet ,chama hicho kilipunguza mikutano yake ya kisiasa ili kutoa nafasi kwa rais Uhuru Kenyatta kutekeleza miradi yake