ODM TRANS NZOIA YAAPA KUSHINDA VITI VINGI VINGI.


Wafuasi wa chama cha ODM Kaunti ya Trans Nzoia wakiongozwa na Moses Masinde wamesema wako tayari kushinda viti vingi kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Akiongea na wanahabari mjini Kitale baada ya kupokea tiketi ya moja kwa moja, Masinde anayewania kiti cha Ubunge katika eneo Bunge la Endebess amepuuzilia mbali madai kwamba ODM haingekuwa na wawaniaji baada ya Raila Odinga kumuunga George Natembeya kuwa Gavana wa muungano wa Azimio la Umoja-One Kenya kaunti ya Trans nzoia.
Hata hivyo Everlyne Nekesa Wasike ambaye ni mojawapo ya viongozi wa kike wanaotafuta viti vya kuchaguliwa katika Wadi ya Chepchoina akipongeza hatua ya chama cha ODM kwa kuweza kutambua jinzia ya Kike huku akisema itakuwa bora iwapo muungano wa Azimio la Umoja -One Kenya utamuteua Martha Karua kuwa Naibu wa Raila Odinga kwenye uchaguzi Mkuu.