ODM POKOT MAGHARIBI YATETEA MWAFAKA BAINA YA KENYATTA NA RAILA.

Na Benson Aswani
Chama cha ODM katika kaunti hii ya Pokot magharibi kimetetea mwafaka baina ya kinara wa chama hicho Raila Odinga na rais Uhuru Kenyatta.
Akizungumza katika mahojiano na kituo hiki muda mfupi uliopita, mwenyekiti wa chama hicho kaunti hii Joseph Akaule amesema kuwa mwafaka huo umesaidia kuhakikisha kuwa taifa linaendeshwa kulingana na matarajio ya mwananchi kwani sasa kinara wa chama hicho yuko karibu na rais ambapo yuko katika nafasi nzuri ya kutoa mchango wake katika uongozi wa taifa.
Aidha akaule amepuuzilia mbali uwezekano wa raila kupendelewa katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao akisema kuwa chama hicho kinategemea kwa kiwango kikubwa kura ya mwananchi.
Aaidha akaule amesema kuwa uhusiano kati ya rais Kenyatta na odinga umepekea kuimarika huduma nchini ikiwemo kupunguza maswala ya ufisadi ambao anadai ulikuwa umekithiri serikalini.