ODM CHAPUUZILIA MBALI MADAI YA KUTOSIMAMISHA WAGOMBEA TRANS NZOIA.


Chama cha ODM kaunti ya Trans nzoia kimekishutumu chama cha DAP K kwa kueneza propaganda kwamba chama hicho hakitasimamisha wagombea viti mbali mbali kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Wakiongozwa na katibu mkuu John Simiyu, viongozi wa chama hicho wamekariri kuwa ODM kitasimamisha wagombea katika nyadhifa zote za kisiasa kaunti hiyo, wakitaka DAP-K kutarajia ushindani baina ya vyama vilivyo chini ya muungano wa azimio la umoja.
Wakati uo huo viongozi hao wamevikaribisha vyama vingine kwenye muungano wa azimio la umoja huku wakivitaka vyama hivyo kuendeleza kampeni zao kutafuta uungwaji mkono kutoka kwa wananchi wala si kutegemea kuachiwa nafasi hizo.