ODM CHAKANA KUWEPO MKATABA KATI YAKE NA KUP.


Mwenyekiti wa Chama Cha ODM katika Kaunti ya Pokot Magharibi Joseph Akaule ameweka bayana kwamba hakujakuwapo na maelewano baina ya Chama hicho na Chama Cha KUP chake gavana John Lonyangapuo.
Wakihojiwa katika kituo wakiwa na Mwenyekiti wa KUP Geofrey Lipale, Akaule amesema licha Kinara wa ODM Raila Odinga kufika katika Kaunti hii ya Pokot Magharibi na kukabidhiwa mahitaji ya jamii ya Pokot, hakuna sahihi imewekwa kuonyesha kwamba KUP kimekubaliwa ndani ya Azimio la Umoja na
Kulingana Akaule KUP kinajipendekeza ndani ya Azimio.
Hata hivyo Mwenyekiti wa KUP Geofrey Lipale amesema japo hakujakuwa na sahihi inayoonyesha kuwa wamejiunga na Azimio, Chama Cha KUP kiko tayari kumtetea Raila Odinga kuwania urais Agosti tisa huku akitaja kwamba muungano wa Azimio la Umoja unahitaji Chama Cha KUP zaidi ya jinsi ambavyo KUP kinahitaji Azimio.