ODM CHAANZA MIKAKATI YA KUJIIMARISHA POKOT MAGHARIBI.


Chama cha ODM kimeanza mikakati ya kuhakikisha kinatwaa viti vingi katika uchaguzi mkuu ujao.
Akizungumza baada ya kikao na viongozi wa chama hicho kaunti hii ya Pokot Magharibi kilichoandaliwa katika afisi za chama mjini Kapenguria, mkurugenzi wa kitaifa wa chama hicho Oduor Ong’wen amesema kwa sasa wanataka kukiimarisha zaidi chama hicho katika kaunti hii ili kupata wafuasi na wengi pamoja na wagombea wa nyadhifa mbalimbali.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama hicho kaunti hii Joseph Akaule ametoa wito kwa wakazi wa kaunti hii kuunga mkono chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao ili kunufaika zaidi kimaendeleo.
Nao Wanachama wa chama hicho kaunti hii ambao pia wametangaza nia ya kugombea nyadhifa mbalimbali kwa tiketi ya ODM wameelezea haja ya kinara wa chama hicho Raila Odinga kupewa nafasi ya kuongoza taifa kutokana na kile wamedai taifa limeafikia mengi kupitia juhudi zake.