OCPD ANAYEONDOKA AMTAKA MRITHI WAKE KUENDELEZA USHIRIKIANO MWEMA POKOT YA KATI.

OCPD wa Sigor kaunti hii ya Pokot magharibi anayeondoka Bamford Surwa amemtaka anayechukua nafasi yake pamoja na maafisa wengine wa usalama eneo hilo kuendeleza ushirikiano mwema alioanzisha baina ya maafisa wa usalama na wananchi.

Akuzungumza baada ya hafla ya kumwaga rasmi Surwa amesema kwamba ni wananchi ndio walio na habari muhimu zinazohusu maswala mbali mbali ambayo huenda yanatafutiwa ufumbuzi na maafisa wa usalama na itategemea ushirikiano iliopo kati ya maafisa hao na wananchi kupata habari hitajika.

Hata hivyo Surwa ambaye amepewa uhamisho hadi eneo la Matete katika kaunti ya Kakamega amesifia utendakazi wa maafisa hao katika kipindi ambacho amehudumu eneo hilo akiwataka kutolegeza kamba na badala yake kuendeleza juhudi hizo.

Aidha Surwa amesema kwamba ako tayari kukabiliana na changamoto ambazo zinahusishwa na mazingira mapya anakotarajiwa kuhudumu akiahidi kuendeleza juhudi za kuhakikisha utendakazi bora wa wote anaoshirikiana nao katika sekta ya usalama.

Aidha Surwa ameelezea baadhi ya changamoyo ambazo alikumbana nazo katika kipindi chake ambacho alihudumu eneo la Sigor ikiwemo maporomoko ya ardhi ambayo yalishuhudiwa mwezi aprili mwaka 2020 ambapo maafisa wawili wa polisi walipoteza maisha yao.