NRT YAPEWA IDHINI YA KUNDELEZA SHUGHULI ZAKE KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI

Wakfu wa umiliki wa wanyamapori NRT utaendelea na shughuli zake mbali mbali katika maeneo mbali mbali ya kaunti hii ya Pokot magharibi baada ya uamuzi wa mahakama kuwapa idhini hiyo japo kwa masharti.
Hii ni baada ya baadhi ya wakazi wa kaunti hii kuwasilisha kesi mahakamani kulizuia shirika hilo kutekeleza miradi yake, mratibu wa shirika hilo Rabecca Chebet akisema kuwa watatekeleza shughuli ambazo wameruhusiwa na mahakama wakati kesi hiyo ikiendelea kusikilizwa.
Akizungumza baada ya kikao cha kufafanua uamuzi huo wa mahakama, kikao ambacho kilihudhuriwa na maafisa wa serikali kuu pamoja na wale wa serikali ya kaunti Chebet ametoa wito kwa wakazi wa kaunti hii kuruhusu shirika hilo ambalo ni mshirimka wa eu kutekeleza miradi hiyo ambayo ni ya kuwafaidi wakazi.
Naibu kamishina wa kaunti hii Kennedy Lunalo ambaye alihudhuria kikao hicho amesema kuwa kilinuia kufafanua uamuzi huo wa mahakama kwa maafisa hao wa utawala.