NRT YAENDELEZA MAFUNZO KWA WAKULIMA POKOT MAGHARIBI.


Shirika la SEFA chini ya Northern Rangelands Trust NRT limeendelea kutoa mafunzo kwa wakulima katika kaunti hii ya Pokot magharibi kuhusu kilimo bora.
Afisa katika shirika hilo Beatrice Hadeny amesema kuwa lengo kuu la mafunzo yanayotolewa kwa wakulima maeneo mbali mbali ya kaunti hii ni kuhakikisha kuwa wakulima wanapanda mimea iliyo na madini yenye manufaa mwilini ili kuafikia lishe bora miongoni kwa jamii.
Aidha Hadeny amesema kuwa shirika hilo linaendelea kuwahimiza wakulima kuhusu umuhimu wa kukumbatia mimea ambayo inafaa maeneo yenye mvua chache kutokana na hali kuwa wengi wa wakulima kaunti hii wameegemea zaidi upanzi wa mahindi.