NHIF YATAFUTA MAONI YA KUIMARISHA HUDUMA ZAKE TRANS NZOIA.
Bima ya kitaifa ya afya NHIF imeandaa kongamano na wahudumu wa umma ili kupata maoni ya jinsi bima hiyo inaendelea kuimarisha huduma yake kwa wafanyakazi wa serikali nchini.
Kwenye mkao na wanahabari baada ya kufungua rasmi kongamano hilo Kamisha wa Kaunti ya Trans Nzoia Sam Ojwang ameelezea umuhimu wa mabadiliko kwenye bima hiyo akisema inaboresha zaidi utoaji wa huduma hiyo mbali na kuhakikisha kuafikiwa kwa ajenda ya serikali ya afya kwa wote.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bima ya NHIF tawi la Trans Nzoia Amos kipkoech amesema Kaunti ya Trans Nzoia imesajili zaidi ya watu 400,000 na kukadiria familia ya watu 1M wanaofaidi bima hiyo akisisitiza kuwa NHIF imeboresha huduma zake ikiwa ni pamoja na bima ya kusimamia matibabu kwenye mataifa ya kigeni kwa kila mwananchi aliye jisajili na bima hiyo.