NG’OLESIA AKANA MADAI KUWA ATAGOMBEA KITI CHA UBUNGE SIGOR.


Mwakilishi wadi ya Seker kaunti hii ya Pokot magharibi Thomus Ng’olesia amekana madai kuwa ananuia kugombea kiti cha ubunge katika eneo bunge la Sigor kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Akizungumza na kituo hiki Ng’olesia ambaye pia ni kiongozi wa wengi katika bunge la kaunti hii ya Pokot magharibi, amekana kutangaza kugombea kiti hicho akisema kuwa atatangaza msimamo wake wa iwapo atagombea kiti hicho au la, wakati mwafaka utakapofika.
Aidha Ng’olesia amesema kuwa uamuzi wake wa kiti atakachogombea katika uchaguzi mkuu ujao, utategemea matakwa ya wakazi wa eneo hilo.
Amesema kwa sasa anazingatia kwanza utekelezaji wa majukumu aliyopewa na wakazi wa wadi ya seker.