NDOA ZA MAPEMA ZAPUNGUA POKOT KASKAZINI.


Visa vya ndoa za mapema vimepungua eneo la Pokot kaskazini katika kaunti hii ya pokot magharibi katika siku za hivi karibuni kutokana na mipango mbali mbali inayoendeshwa eneo hilo na mashirika ya kijamii kwa ushirikiano na viongozi mbali mbali wa utawala.
Haya ni kulingana na kamanda wa polisi pokot kaskazini Nathan Sanya, ambaye amesema licha ya kuwa vipo baadhi ya visa vinavyoripotiwa mara moja moja, mipango ambayo inaendeshwa na serikali kwa ushirikiano na mashirika kama vile world vision miongoni mwa mengine imechangia pakubwa kupunguza visa hivyo.
Aidha sanya amesema kuwa viongozi wa usalama eneo hilo wameweka mikakati ya ushirikiano na wenzao wa kutoka taifa jirani la Uganda, kuhakikisha kuwa hamna mtoto wa kike kutoka pande zote mbili anayetoroshwa ili kuolewa pande hizo.
Wakati uo huo Sanya amewataka wazazi eneo hilo ambao wanao wamejifungua kuwarejesha shuleni ili kuendelea na masomo na kuafikia ndoto yao maishani, huku akionya vikali watakaopatikana na kuhusika na visa vya kuwaoa wanafunzi.