NDOA ZA MAPEMA NA UKEKETAJI WASALIA CHANGAMOTO KWA ELIMU YA MTOTO WA KIKE.

Na Benson Aswani
Swala la mimba za mapema pamoja na ukeketaji kwa mtoto wa kike kaunti hii ya Pokot magharibi limesalia changamoto kuu kwa elimu ya mtoto wa kike licha ya juhudi ambazo zimewekwa kuhakikisha kuwa swala hilo linakabiliwa.
Haya ni kulingana na mwakilishi wa walimu wa kike katika chama cha walimu wakuu wa shule za msingi kanda ya rift valley Kepsha ambaye pia ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Nasokol Cecilia Ngige ambaye ametoa wito kwa wadau kuzidisha juhudi za kukabili uovu huu ili kumpa fursa mtoto wa kike pia kuafikia ndoto yake maishani.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na OCS wa kituo cha polisi cha Kacheliba Tom Nyanaro ambaye amesema kuwa licha ya kuwa maafisa wa usalama wanajitahidi kuhakikisha mtoto wa kike analindwa dhidi ya ndoa za mapema na ukeketaji vita hivyo havitafaulu pasi na ushirikiano kutoka kwa wadau.