NDMA YAENDELEZA UTATHMINI WA ATHARI ZA MSIMU WA MVUA POKOT MAGHARIBI.


Mamlaka ya kushughulikia majanga NDMA katika kaunti hii ya Pokot magharibi inaendeleza utathmini wa athari za msimu wa mvua uliokamilika ili kubaini athari za mvua hiyo katika sekta mbali mbali kaunti hii.
Akizungumza baada kikao cha kuangazia hatua ambazo zimepigwa wiki moja tangu kuanza utathmini huo, mshirikishi wa NDMA kaunti hii Michael Kimiti amesema kuwa wanalenga zaidi athari za msimu huo katika uzalishaji wa chakula, mifugo, lishe pamoja na sekta ya elimu.
Kimiti amesema kuwa data ambazo zitakusanywa kutoka maeneo mbali mbali ya kaunti hii ya Pokot magharibi zitatumika kubaini viwango vya athari zilizosababishwa na msimu wa mvua kwa watu binafsi au sekta mbali mbali ili kutathmini msaada utakaohitajika kutolewa kwa watu au sekta athirika.
Ni utathmini unaojiri wakati idara ya utabiri wa hali ya anga kaunti hii ya Pokot magharibi ukiashiria kuendelea kushuhudiwa vipindi vya jua mwezi huu wa februari, maeneo kadhaa yakitarajiwa kushuhudia mvua chache hasa katika nyanda za juu.
Wilson Lonyang’ole ni mkurugenzi wa idara ya utabiri wa hali ya anga kaunti hii.