NCIC YATAKIWA KUFUATILIA MIENENDO YA WANASIASA TRANS NZOIA.


Tume ya kitaifa ya uwiano na utangamano wa kitaifa NCIC na idara ya upelelezi DCI zimetakiwa kufuatilia kwa karibu viongozi wa kisiasa ambao wanatoa semi za chuki katika mikutano mbali mbali ya kisiasa ili kuwatia nguvuni na kuwafungulia mashitaka.
Wakiongozwa na mwakilishi maalum Margaret Wanjala, viongozi wa kike katika kaunti ya Trans nzoia wamesema kuwa kila mwanasiasa ana uhuru wa kutangaza sera zake na kuwashawishi wapiga kura pasi na kuwachochea kwa misingi ya kikabila au eneo anakotoka.
Wanjala ambaye ametangaza nia ya kugombea kiti cha mwakilishi wa kike kaunti ya Trans nzoia katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao amewataka wakazi wa kaunti hiyo kuishi kwa amani huku akirejelea kauli yake aliyekuwa rais hayati Daniel Toroitich Arap Moi kuwa siasa mbaya maisha mabaya.