NCIC YATAKIWA KUFUATILIA KWA MAKINI KAULI ZA WANASIASA MSIMU HUU WA KAMPENI ZA UCHAGUZI.
Tume ya uwiano na utangamano NCIC imetakiwa kufuatilia mienmendo ya viongozi wa kisiasa nchini na kuwachukulia hatua kali wanasiasa ambao wanawachochea wananchi wakati huu taifa linapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi agosti mwaka huu.
Wakiongozwa na katibu Meshack Kosgei, viongozi wa kidini katika kaunti ya Trans nzoia chini ya baraza la madhehebu nchini wamesema kuwa wapo wanasiasa ambao wameanza kutumia semi za chuki hasa katika mikutano yao ya kampeni hali wanayosema inapasa kukomeshwa kabla ya kufika katika viwango visivyothibitika.
Wakati uo huo Viongozi hao wamelalamikia kile wanachosema kudhulumiwa kina mama na watu wanaoishi na changamoto za ulemavu wakati wanapoendesha kampeni zao, wakishinikiza usawa miongoni mwa wanasiasa wote katika kampeni hizo.