NATEMBEYA ATANGAZA KUJIUZULU JUMA HILI.

NA BENSON ASWANI
Mshirikishi wa utawala eneo la bonde la ufa George Natembeya ametangaza kuwa atajiuzulu kutoka wadhifa wake juma hili ili kujitosa rasmi katika ulingo wa kisiasa kuwania ugavana wa kaunti ya Trans nzoia katika uchaguzi mkuu wa mwezi agosti mwaka huu.
Akizungumza mjini Kitale Natembeya amewataka wapinzani wake kuwa tayari kwa kinyang’anyiro kikali huku akiwaahidi wakazi wa kaunti hiyo ya Trans nzoia kutarajia huduma bora iwapo atachaguliwa gavana wa kaunti hiyo.
Wakati uo huo Natembeya amewataka wakazi wa kaunti hiyo kuwa makini katika uchaguzi mkuu ujao na kuwapiga msasa viongozi wote ambao wametangaza nia ya kugombea nyadhifa za kisiasa ili kuwachagua viongozi ambao watakuwa tayari kuwahudumia inavyopasa.